MKUU wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego amewataka wazazi na walezi wilayani tanga kuwapatia watoto wao elimu bora kutokana na kuwepo kwa tabia ya wazazi na walezi kutokuwa na moyo wa kusimamia elimu za vijana wao sasa msikilizaji una maoni gani kulingana na agizo hilo la mkuu wa wilayaa ya Tanga na nini mtazamo wako katika hili?ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.
Dendego
ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza kwenye mahafali ya
kwanza ya shule ya sekondari ya wavulana ya Elohim yaliyofanyika shuleni hapo.
Amesema
suala la elimu sio la kufumbiwa macho bali linapaswa kupewa kipaumbele ikiwemo
wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao lengo likiwa ni kuwapa msukumo wa
kupenda kusoma.
Ameongeza
kuwa watoto wanapopatiwa elimu itaweza kuwakomboa na kuwapa maarifa ya
kuendesha maisha yao vizuri ikwemo kusaidia jamii ambazo zinawazunguka.
Mkuu
huyo wa wilaya ameeleza kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na shule binafsi ili waweze kuchangia maendeleo ya elimu wilayani
hapa.
Katika
hatua nyengine wakati akisoma hotuba yake kwenye mahafali hayo,Dendego amempa
muda wa siku kumi na nne Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Juliana
Malange kumuonyesha barabara ya kufika shuleni ya sekondari ya Elohim iliyopo
eneo la Mwahako jijini Tanga.
Kauli
hiyo inatokana na eneo hilo kutokuwa na barabara nzuri ya kupita wakati wa
kwenda shuleni hapo kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu wazazi na walezi
wanaotaka kwenda shuleni hapo kuwatembelea watoto wao.
No comments:
Post a Comment