Msomaji wa Blog hii huu
siku kama nne tulikuaandikia habari kuhusiana na mkuu wa wilaya ya Tanga Bi Halima
Dendego kuwaasa wanafunzi wakike kutoshiriki vitendo vya ngono ili hali wakiwa
shuleni kwani kufanya hivyo kutawalekea kuto fanya vizuri katika masoma yao
sasa wakati hayo yakijiri shirika lisilokuwa la kiserikali jijini Tanga la Tree
of hope limepanga kuwasaidia wanafunzi kisaikologia baada ya SHULE ya Sekondari
Nguvumali iliopo jijini Tanga, kunadaiwa kukumbwa na pepo la ngono.
Mkurugenzi wa Tree of
Hope, Fortunata Manyeresa, ameahidi kuingia mtaa kwa mtaa kuwasaka wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo ili
wanaowarubuni wachukuliwe hatua.
Hatua hiyo inakuja baada
ya wanafunzi wake shuleni hapo kubainika wakifanya ngono hovyo chooni,
madarasani na njiani wakati wa kwenda na
kurudi kwenye makazi yao.
Hali hiyo inadaiwa
kusababishwa na kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo.
Tatizo hilo liliwekwa
hadharani jana na Diwani wa Kata ya Nguvumali, Mustafa Seleboss na Mwenyekiti wa Nguvumali Agness Milambo,
kwenye bonanza la kampeni za uzinduzi wa kupinga ukatili mashuleni
lililoandaliwa na asasi ya kiraia ya Tree of Hope ya jijini Tanga.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti, viongozi hao wa Kata ya Nguvumali, walisema asilimia 80 ya
wanafunzi wa Sekondari ya Nguvumali wanafanya mapenzi hovyo hata darasani, vyooni
na vichakani wakati wakienda au kurudi nyumbani.
Baadhi ya
wanafunzi shuleni hapo, Peter Chambai,
Hassan Saidy na Teresia John, wamekiri kufanyika kwa vitendo hivyo viovu,
ambavyo wameviita ni ukatili na unyanyasaji
wa kisaikolojia dhidi ya wanafunzi wasiopenda mchezo huo mchafu.
Wanafunzi hao wamesema
washiriki wa vitendo hivyo ni wanafunzi kwa wanafunzi au walimu kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment