Pichani ni mkuu wa shule ya Maramba sec iliyopo Maramba Wilayani Mkinga Magdalena Wandi
MWANAFUNZI wa kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Maramba, Joseph Charles ameshindwa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili baada ya kutuhumiwa kumpiga mwalimu wa shule hiyo wakati wa kazi ya kupanga viti kujiandaa na mitihani hiyo iliyoanza Oktoba4mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya mwanafunzi huyo kufanya vurugu wakati wakipanga viti na kuamua kumpiga mwalimu huyo hali iliyosababisha Jeshi la Polisi kuzingira shule hiyo ili kuzuia vurugu zilizojitokeza.
Mkuu wa Shule hiyo, Magdalena Wandi amesema baada ya tukio hilo kamati ya nidhamu ya shule imemsimamisha masomo mwanafunzi huyo na kushindwa kufanya mtihani huo wa taifa.
Mwalimu
Wandi amesema uamuzi zaidi wa kumwadhibu mwanafunzi huyo kwa tukio hilo la
utovu wa nidhamu litafikiwa hadi hapo bodi ya shule hiyo itakapo kaa.
Aidha
Mkuu huyo wa shule ametoa wito kwa wazazi kuacha tabia ya kuwatetea watoto wao
wanapokuwa wanafanya makosa kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma
harakati za kuboresha elimu hivyo amewataka kuungana kwa pamoja kuinua kiwango
cha elimu kwa kuwapa maadili mema watoto wao.
No comments:
Post a Comment