Search This Blog

Monday, October 21, 2013

MRADI WA NYUMBA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAZINGARA KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI



MRADI wa ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mazingara wilayani Handeni mkoani Tanga ulioanza kutekelezwa kwenye mwaka wa fedha 2013-2014 kwa fedha za maendeleo pamoja na nguvu za wananchi unatarajiwa kukamilika desemba mwaka huu.

Akizungumza hivi karibuni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni,Dr.Khalfani Haule na kusema kuwa ujenzi huo mpaka utakapokamilika utagharimu kiasi cha sh.milioni 25,384,500.
Haule amesema mpaka sasa fedha zilizopokelewa ni sh.15,000,000 na zimetumika sh.12,500,000 ambazo zilifanyia kazi mbalimbali katika hatua ya awali ya ujenzi huo.

Mkurugenzi huyo amezitaja kazi ambazo zimekwisha kutekelezwa kwenye mradi huo ni uchimbaji msingi na kuujenge,kumwaga jamvi ,kujenga boma,kuweka linta na kujenga gebo.
Amezitaja kazi nyengine zilizofanyika ni kupanua na kuezeka,kufitisha ikiwemo kuweka fremu za madirisha na milango pamoja na kufanya kazi ya umaliziaji.

Ameongeza kuwa mpaka hatua iliyofikiwa na mradi huo nguvu za jamii zilizochangwa ni kiasi cha sh.300,000 wakati mradi huo ukitarajiwa kukamilika ifikapo desemba mwaka huu.
Mkurugenzi amesema mradi wa ujenzi nyumba hizo za walimu unatarajiwa kupunguza mahitaji ya nyumba kutoka kutoka kumi na mbili mpaka kufikia kumi na moja kwa walimu wasiokuwa na nyumba.




No comments:

Post a Comment