NA OMARY MLEKWA,HAI
WATANZANIA wametakiwa
kujitokeza katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu ili kuwapatia fursa ya kupata elimu sawa na watoto wasiokuwa na
ulemavu badala ya kutegemea serikali pekee
Akizungumza katika
ziara ya kutembelea watoto wenye ulemavu wa akili katika kata ya Machame
Mashariki, katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa akili wilayani Hai,
Anjella Mallya hali ya miuondo mbinu katika shule nyingi hapa nchini hairuhusu
kuwapa fursa watoto wenye ulemavu
Alisema hali hiyo
imesababishwa na jamii kuwatenga na kuwabagua wenye ulemavu katika suala nzima
la kielimu kwa kutegemea serikali pekee katika kukabiliana na tatizo hilo jambo
ambalo limekuwa likichangia zaidi watoto wengi kushindwa kupata haki zao za
msingi katika elimu
“Ni jukumu letu sote kuwatazama watu wenye
walemavu kama watu wengine na tusiwachife watoto wenye ulemavu badala yake
jamii ihakikishe inaboresha mangira ya watoto hao kwa kina kama ilivyo kwa
watoto wengine ”alisema Mallya
“Tuwasaidie na kuwajali
kwa kuhakikisha wanapata elimu katika
mazingira rafiki, ili
waweze kuchagia maendeleo katika taifa kwani nao wana uwezo wa kujitegemea
iwapo tutawaunga mkono, bila kusahau kuwa ulemavu hauombwi wala kununuliwa bali
unakuja tu,” alisisitiza .
Alisema endapo jamii
ikishirikiana na Serikali kuwa na majengo maalumu ya kwa ajili ya watoto wenye
ulemavu itasaidia kuwavutia watoto hao kusoma kwani mazingira wanayosemea
katika shule za kawaidia yamekuwa si rafiki nao
No comments:
Post a Comment