Search This Blog

Thursday, October 3, 2013

MKUU WA WILAYA YA TANGA AWAPA SOMO WANAFUNZI


























Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego Katikati

Na Oscar Assenga Tanga


MKUU wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego amewataka wanafunzi wa kike katika shule za sekondari wilayani hapa kujitambua na kuacha kufikiria masuala ya mapenzi badala yake watilie mkazo elimu kwani ndio mkombozi wao wa maisha yao ya baadae na familia zao.

Mkuu huyo wa wilaya aliweza kutoa somo la kuwakumbusha wanafunzi hao wakati wa maadhimisho ya wiki ya uwt ambapo kiwilaya yaliadhimishwa kata ya pongwe wilayani hapa na kwatakuwa wazalendo wa kuipenda nchi yao ,kujitambua wao kama vijana wa kike wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupenda elimu na kuachana kufanya ngono zembe ambayo itaweza kuwapelekea kushindwa kutimiza malengo yao.

“Ukisoma utaheshimika na kuweza kufanya kazi yoyote kwa sababu una elimu ikiwemo kuweza kuendesha maisha yao hivyo nawasihii msome kwa bidii na mafanikio yake mtayaona “alisema DC Dendego.

Alisema endapo watasoma kwa bidii kwa kuzingatia yale yote watakayofundishwa darasani watapata uelewa mzuri wa kufanya vizuri katika mitihani yao na hatimaye kuweza kupata kazi nzuri ili kuweza kuzisaidia jamii zao kwa ujumla.

"Nimeunda kikosi kazi cha kuwatafuta wanafunzi wanaotoroka shuleni muda wa masomo ili kuweza kutokomeza vitendo vya wanafunzi kutoroka na hii nadhani itachochea wanafunzi kupenda masoma na kuongeza kasi ya ufaulu miongoni mwao "Alisema DC Dendego.

Aidha katika hatua nyengine mkuu huyo wa wilaya aliwataka wakina mama kujitambua kwa kuongeza jitihada zao katika shughuli za maendeleo kwani wanawake wakiwezeshwa wanaweza hivyo wahakikisha wanakuwa mstari kwa kuungana pamoja ili waweze kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment