JUMLA ya watoto wakike 1,056 wameacha masomo ya shule ya msingi
kutokana na mimba zilizosababishwa na mazingira magumu wanayoishi zikiwamo tamaduni
mbalimbali za makabila.
Takwimu hiyo ilitolewa
jana na Mtaalamu wa Maendeleo ya Jamii, Rosely Kaihula wa Mfuko wa Maendeleo ya
Watoto Ekama, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya mtoto wa
kike duniani itakayoadhimishwa Oktoba 11, mwaka huu.
Mtaalamu huyo amesema
sababu zingine ni mazingira magumu ikiwamo kutokuwa na kipato kwa wazazi ama
walezi pindi mtoto anapohitaji mahitaji muhimu hali inayomsabaisha arubuniwe na
hatimaye kujikuta na ujauzito.
Mratibu wa masuala ya
Familia wa Shirika la SOS Children’s Villages, Magdalena George, alisema lengo
la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa jamii juu ya masuala mbalimbali
yanayomsibu mtoto wa kike, na yataishirikisha serikali, watoto na NGO’s
mbalimbali.
Maadhimisho ya mwaka
huu ambayo yatafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa
na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
Anna Maembe, yatakuwa na kaulimbiu inayosema: “Chochea ubunifu kuboresha elimu
ya mtoto wa kike.”
No comments:
Post a Comment