Search This Blog
Monday, October 28, 2013
KAMA ULIMIS PICHA NA MATUKIO YA MAHAFALI YA SHULE YA WASICHA YA ST.CHRISTIINA CHEKI HAPA BAADHI YA SHOW ZILIZOFANYIKA
Sunday, October 27, 2013
PICHA NA MATUKIO TOFAUTI YA MAHAFALI YA 9 YA SHULE YA WASICHANA YA ST.CRISTINA
MAANDAMANO YA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE YA SHULE YA WASICHANA YA ST .CRISTINA |
MEZA KUU |
BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU WAKIIMBA WIMBO WA TANZANIA TANZANIA |
MKUU WA SHULE YA WASICHANA YA ST CRISTINA MWALIMU SINGANO AKIZUNGUMZA MACHACHE KUHUIANA NA SHULE HIYO |
BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU WAKITOA BURUDANI YA NGOMA |
KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA PANGANI BI HAFSA MTASIWA MEZA KUU AKIPERUZ MACHACHE |
DR.NDELAKINDO KESSY MBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KWENYE MAHAFALI HAYO |
BAADHI YA WALIMU WA SHULE YA WASICHANA YA ST.CRISTINA |
MGENI RASMI AKIKABIDHI ZAWADI NA VYETI KWA BADHI YA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI |
Wednesday, October 23, 2013
PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA UZINDUZI WA MAABARA YA SHULE YA LIVING STONE MUHEZA
MKUU WA MKOA WA TANAGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALAWA KUSHOTO,KULIA NI MOJA KATI YA WALIMU WA SHULE HIYO KUTOKA KOREA |
MKUU WA MKOA WA TANGA AKIZINDUA JENGO MAAMBARA |
MKUU WA MKA WA TANGA AKISOMEWA TAARIFA FUPI YA SHULE HIYO |
BAADHI YA WANAFUNZI WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA SHULE HIYO WAKIWA TAYARI KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA TANGA SHULENI HAPO.picha zote kwa hisani ya blog ya Tanga Raha |
Monday, October 21, 2013
HALMASHAURI MKOANI TANGA ZAAGIZWA KUJIKITA ZAIDI KWENYE UJENZI WA MAABARA ZA SHULE
NA OSCAR ASSENGA TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ameziagiza
Halmashauri zote mkoani hapa kuelekeza msukumo mkubwa kwenye ujenzi wa maabara
tatu kila shule ili kuwawezesha wanafunzi kupenda kusoma masomo ya sayansi na
kuweza kufanya vizuri.
Gallawa ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea
shule ya seminari ya wavulana ya Livingstone iliyopo wilayani hapa pamoja na kuzindua
jengo la maabara ya kompyuta iliyojengwa
kwa thamani y ash. 149,000,000 ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ndani.
Amesema ujenzi huo wa maabara kwa vyumba vitatu kila
shule ni agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete hivyo kuzitaka halmashauri hizo kutilia mkazo suala hilo kwenye maeneo
yao.
Ameongeza kuwa maabara hizo zinapaswa kuwepo kwenye
shule za sekondari kuanzia za kata na zile za binafsi kwani hakuna maendeleo
yanayoweza kupatikana bila ya kuwepo wanasayansi.
Aidha amesema katika hilo inabidi itumike nguvu
kubwa ikiwemo hata kuhairisha miradi mengine ili kuzielekeza kwenye ujenzi wa
maabara kwenye shule hizo.
“Halmashauri
zote zinatakiwa kujenga maabara tatu tatu kila shule na sio mbili kwani hilo ni
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
Amezitaka halmashauri kupitia ofisa elimu kupita
kwenye shule za binafsi kuwasisitizia suala hilo la ujenzi wa maabara kwani ni
muhimu sana hasa kwenye maendeleo ya nchi yetu.
Mkuu huyo wa mkoa ameziagiza pia shule za sekondari
na msingi mkoani hapa kupanda zao la mkonge kwenye mipaka yao ili kuwezesha
wanafunzi kufundishwa jinsi ya kupanda zao hilo.
PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI ELOHIMU
MKU WA WILAYA TANGA HALIMA DENDEGO AKIONESHWA BAADHI YA VIFAA VINAVYOTUMIKA KATIKA MAABARA YA SHULE HIYO KALBA YA MAHAFALI KUANZA |
MKURUGENZI WA SHULE YA ELOHIMU BOYS BI ELINGAYA MUNGURE AKITOA HOTUBA YAKE KWA MGENI RASMI |
MKUU WA WILAYA YA HALIAMA DENDEGO AKITOA MAELEKEZO KWA WANAFUNZI |
BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WA SHULE YA WAVULA NA YA ELOHIMU BOYS WAKIFANYA VITU VYAO |
PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA KIDATOCHA NNE MLALO SEKONDARI
KATIBU WA UENEZI WA CCM WILAYA YA KOROGWE BW.RICHARD MGANGA ALIYEMUAKILISHA MWENYEKITI WA CCM MKOA KATIKA MAHAFALI HAYO KUSHOTONI MKUU WA SHULE HIYO SUFIANI SHEKOLOLA |
BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAKIONESHA VITU VYAOMBELE YA MGENI RASMI |
MMOJA WA WALIMU WANAOFUNDISHA SHULENI HAPO BW SULTANI |
KATIBU WA UENEZI CCM WILAYA YA KOROGWE BW..MGANGA KUSHOTO,KULIA NI MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM WILAYANI LUSHOTO WAKIENDESHA HARAMBEE SHULENI HAPO |
BAADHI YA WATU WALOHUDHURIA MAHAFALI HAYO |
ELIMU BADO CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI ELOHIMU BOYS
Licha
ya shule ya sekondari ya wavulana ya Elohim kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma
inakabiliwa na changamoto ya wanafunzi wengi kushindwa kujitambua na kuona suala zima la kusoma kama mzingo
waliotishwa na wazazi wao.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Jofrey Makanza wakati akisoma
hotuba yake kwa mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego kwenye mahafali ya
kwanza ya kidato cha nne ya shule hiyo.
Makanza
amesema suala lengine ambalo limekuwa kikwazo kwao ni wazazi,walezi kushindwa
kulipa ada zao kwa wakati na kueleza jinsi wanavyokabiliana nayo likiwemo la
kuwakumbusha wazazi kutimiza wajibu wao ikiwemo kuwarudisha nyumbani.
Amesema
wanafunzi wanaoshindwa kuonesha uendelevu wa kitaaluma kwa kiwango
kinachostahili hupewa ushauri unaostahili na walimu wakishirikiana na wazazi
wao ili kupata wahitimu bora na sio bora wahitimu sanjari na mkakati wa
serikali wa Big result now.
Aidha
ameishukuru serikali kwa mikakati mbalimbali ya kielimu inayoiweka ili kuinua
kiwango cha ufaulu kwa watoto hususani kurejeshwa mitihani ya kidato cha pili.
MRADI WA NYUMBA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAZINGARA KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI
MRADI
wa ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari Mazingara wilayani
Handeni mkoani Tanga ulioanza kutekelezwa kwenye mwaka wa fedha 2013-2014 kwa fedha
za maendeleo pamoja na nguvu za wananchi unatarajiwa kukamilika desemba mwaka
huu.
Akizungumza
hivi karibuni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni,Dr.Khalfani Haule
na kusema kuwa ujenzi huo mpaka utakapokamilika utagharimu kiasi cha sh.milioni
25,384,500.
Haule
amesema mpaka sasa fedha zilizopokelewa ni sh.15,000,000 na zimetumika
sh.12,500,000 ambazo zilifanyia kazi mbalimbali katika hatua ya awali ya ujenzi
huo.
Mkurugenzi
huyo amezitaja kazi ambazo zimekwisha kutekelezwa kwenye mradi huo ni uchimbaji
msingi na kuujenge,kumwaga jamvi ,kujenga boma,kuweka linta na kujenga gebo.
Amezitaja
kazi nyengine zilizofanyika ni kupanua na kuezeka,kufitisha ikiwemo kuweka
fremu za madirisha na milango pamoja na kufanya kazi ya umaliziaji.
Ameongeza
kuwa mpaka hatua iliyofikiwa na mradi huo nguvu za jamii zilizochangwa ni kiasi
cha sh.300,000 wakati mradi huo ukitarajiwa kukamilika ifikapo desemba mwaka
huu.
Mkurugenzi
amesema mradi wa ujenzi nyumba hizo za walimu unatarajiwa kupunguza mahitaji ya
nyumba kutoka kutoka kumi na mbili mpaka kufikia kumi na moja kwa walimu
wasiokuwa na nyumba.
WAZAZI WATAKIWA KUWAPATIA WATOTO WAO ELIMU BORA
MKUU wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego amewataka wazazi na walezi wilayani tanga kuwapatia watoto wao elimu bora kutokana na kuwepo kwa tabia ya wazazi na walezi kutokuwa na moyo wa kusimamia elimu za vijana wao sasa msikilizaji una maoni gani kulingana na agizo hilo la mkuu wa wilayaa ya Tanga na nini mtazamo wako katika hili?ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.
Dendego
ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza kwenye mahafali ya
kwanza ya shule ya sekondari ya wavulana ya Elohim yaliyofanyika shuleni hapo.
Amesema
suala la elimu sio la kufumbiwa macho bali linapaswa kupewa kipaumbele ikiwemo
wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao lengo likiwa ni kuwapa msukumo wa
kupenda kusoma.
Ameongeza
kuwa watoto wanapopatiwa elimu itaweza kuwakomboa na kuwapa maarifa ya
kuendesha maisha yao vizuri ikwemo kusaidia jamii ambazo zinawazunguka.
Mkuu
huyo wa wilaya ameeleza kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na shule binafsi ili waweze kuchangia maendeleo ya elimu wilayani
hapa.
Katika
hatua nyengine wakati akisoma hotuba yake kwenye mahafali hayo,Dendego amempa
muda wa siku kumi na nne Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Juliana
Malange kumuonyesha barabara ya kufika shuleni ya sekondari ya Elohim iliyopo
eneo la Mwahako jijini Tanga.
Kauli
hiyo inatokana na eneo hilo kutokuwa na barabara nzuri ya kupita wakati wa
kwenda shuleni hapo kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu wazazi na walezi
wanaotaka kwenda shuleni hapo kuwatembelea watoto wao.
Subscribe to:
Posts (Atom)