Search This Blog

Monday, December 30, 2013

IDARA YA UKAGUZI IBORESHWE KUNUSURU ELIMU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu (CCM          
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Betty Machangu (CCM), ameishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuangalia na kuboresha Idara ya Ukaguzi ili kuipa makali ili itembelee na kukagua shule zilizopo mikoani na siyo kuishia mijini.

Akizungumza na wandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Machangu alisema kama serikali inataka kukuza kiwango cha elimu, ni lazima iangalie namna ya kuboresha ukaguzi kwani ndiyo roho ya elimu nchini.
“Watu wanaongea kuhusu mitaala ya elimu na mambo mengine ila nataka kuwaambia kama Idara ya Ukaguzi kama haitapewa fedha za kutosha ili iweze kwenda vijijini ni sawa na bure,” alisema Machangu.

Machangu alisema: “Ukifutilia shule nyingi hapa nchini utakuta zina vyoo visivyokuwa na uwezo kutumiwa na binadamu pamoja na walimu kutoudhuria madarasani, yote hayo yanachangia elimu kushuka na tusitegemee miujiza katika elimu.”

Machangu alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku nne tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu.
SOURCC Nipashe

Sunday, December 15, 2013

PICHA ZA MAHAFALI YA 19 DSJ HIZI HAPA

Meza kuu
Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka hu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawaziliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.

Baadhi ya wahitimu wakibadilishana mawili matatu


Dotto, Abushehe Nondo, Ibrahim Yamola na Juliana Malondo



Sunday, December 1, 2013

SHULE 10 SEKONDARI ARUSHA ZAULA TEKNOHAMA















Shule 10 za sekondari za serikali mkoani hapa zinatarajiwa kuunganishwa bure na huduma za intaneti yenye kasi ya 4G LTE  ili  kuinua uelewa wa wanafunzi katika somo la Teknolojia ya Habari (Teknohama).

Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mtandao wa huduma za Fouth Generation Long Term Evolution jijini hapa, mkurugenzi  wa kampuni Smile Communication kwa Tanzania na Uganda, Fiona Mcgloin, alisema kwa

kuanzia wamewaunganishia huduma hiyo Shule ya Sekondari ya Arusha baada ya uzinduzi uliofanyika juzi.

Alisema kama sehemu ya mpango wa kuwajibika kijamii wa kampuni hiyo, inatoa huduma za bure za intaneti yenye kasi katika shule za serikali na kwamba hadi sasa shule 10 za jijini Dar es Salaam zinanufaika na huduma hiyo na kuna mpango kama huo kufanyika mkoani hapa.

Aidha alisema wanatarajia kufanya hivyo kwa mikoa yote ambayo watakayozindua huduma hiyo.

Alisema wapo tayari kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya biashara zilizopo mkoani hapa na kuwapa kazi wakazi wa jiji.

Alisema mtandao huo utawasaidia wafanyabiashara, watalii na sekta ya elimu ambayo kwa kiasi kikubwa Arusha imekuwa kitovu.

Alisema Smile ilizinduliwa Dar es Salaam Mei 16, mwaka huu na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mapinduzi haya ya teknolojia.

Katika sekta inayokua kwa kasi ya mawasiliano hapa nchini, intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara nne zaidi kuliko 3.75G.
Source Nipashe

Tuesday, November 26, 2013

NIKI WA PILI ASEMA NENO KUHUSU WANAFUNZI!

Raper artist kutoka kundi la weusi Niki wa pili amewataka wanafunzi Tanzania kusoma kwa bidii na kutokata tamaa ya kimaisha.

Kauli hiyo ya niki wa pili inakuja baada ya kuulizwa swali juu ya nini anafikiri mara baada ya kumaliza degree yake ya pili ya Managment devolopment wiki iliyopita.

Niki amewataka wanafunzi kutambua umuhimu wa elimu licha ya kuwa wengi hukata tamaa kutokana na mikakati yao kuwa katika hali duni.

Hata hivyo niki amesema kusoma si kugumu na kinachotakiwa ni kupenda na kuweka juhudi kwa kuzingatia uchaguzi sahihi wa masomo wa mwanafunzi atakayoweza kuyamudu.

 "Uki sooma elimu itakupa uwanja mpana katika maisha yako na itakuongezea heshima na thamani ya maisha yako"Alisema niki wa pili

Niki ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum kupitia kituo cha redio mwambao fm Tanga mapema hii leo kupitia kipindi cha mimi na mwanafunzi kinarushwa redioni hapa.

Saturday, November 23, 2013

MWASITY AWATOA HOFU WANAFUNZI TANGA



































Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mdau wa mausuala ya elimu hapa nchini Mwasiti Almas a.k.a mwasiti amewatoa hofu wanafunzi wa mkoa wa Tanga juu ya kuchelewa kwa tour za kampeni ya tokomeza zero.

Mwasity ametoa kauli hiyo  kutoka na kuonekana kuchelewa kwa tour za kampeni hizo zilijulikanazo kama tokomeza zero.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu kwenye kipindi cha Mimi na Mwanafunzi kinachorushwa na Redio Mwambao fm ya Tanga Msanii huyo amesema kampeni hiyo ya uhamasishaji na uelimishaji juu ya wanafunzi kusoma kwa biidii na kuepuka matokeo mabaya inaendelea.

Hata hivyo mwasiti amesema safari za kuzunguka kwa ajili ya uhamasishaji na ulimishaji juu ya kampeni hiyo mashuleni zimechelewa kuanza mapema kutokana na wasanii walioshiriki katika kampeni hiyo wengi kumalizia project zao mbalimbali za kimziki mwishoni mwa mwaka na kampeni hiyo itaanza rasmi mwezi januari.

Aidha amewataka wanafunzi mkoani Tanga kusoma kwa bidii na kuwa tayari kwa ajili ya kampeni hiyo itakayo ambatana na utambuzi wa makundi mbalimbali ya wanafunzi watakayo yatengeneza kwa ajili ya uhamasishaji na uelimishaji juu ya kampeni hiyo..

Wednesday, November 20, 2013

WALIMU WAJA NA MBINU MPYA


 Baadhi ya walimu mkoani Tanga wamebuni namna mpya ya kuwafundisha wanafunzi wao kirahisi baada ya vitabu vya somo husika kuwa vichache chek hii hapa walimu wameamua kuandika table ya somo la chemisrty ukutani ili kuwapa wanafunzi unafuu zaidi wa kukariri
HAYA WALE WAKALI WA CHEMISTRY

Monday, November 18, 2013

SHULE ZAKOSA VYOO BABATI


SHULE  za msingi za Qash na Dudiye zilizopo wilayani Babati mkoani Manyara zimetajwa kutokuwa na vyoo tangu mwaka 2006 hadi sasa na badala yake wanafunzi mapori yaliyo jirani na shule kwa ajili ya kujisaidia.

Hayo yamebainika wakati wa kikao cha mrejesho wa kampeni ya ya uwajibikaji jamii ilichoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Eraston Mbwilo ni baada ya maofisa wa Shirika la Haki elimu kutembelea baadhi ya shule za msingi wilayani humo na kujionea hali halisi katika shule hizo.

Akitoa marejesho katika kampeni hiyo, Asia Lembariti amesema kwamba shule hizo hazina matundu ya vyoo tangu mwaka 2006 hadi sasa hali ambayo inatia wasiwasi kwa kuibuka kwa magonjwa ya kuhara na kichocho.

Nae Ofisa Elimu wa Shule za msingi, Mery Consolata amekiri kutokuwepo kwa miundo mbinu katika shule hizo hasa vyoo,vyumba vya madarasa na walimu na kusema kwamba wazazi na walimu wanapaswa kushirikiana ili kuweza kuondokana hali hiyo ya muda mrefu.

BODI YA MIKOPO YATAKIWA KUONGEZA KASI ZANZIBAR


Na masanja Mabula Zanzibar
Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu Zanzibar imetakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni kutoka kwa wahitimu waliokopeshwa na Bodi hiyo ili kuongeza uwezo wa Bodi kutoa mikopo zaidi kwa wanafunzi.

Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati akihitimisha Kikao cha Kutathmini Utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwaka 2012/2013 na robo ya kwanza ya mwaka 2013/2014.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo katika bajeti ya mwaka wa fedha uliopita zilihitajika jumla ya shilingi bilioni 7.7 kulipia wanafunzi 1012 wa zamani na wanafunzi wapya 881 pamoja na madeni ya nyuma.

Kwa upande wa mwaka wa fedha 2013/2014 taarifa imeonyesha kuwa Bodi hiyo imeweza kuwadhamini wanafunzi 1,300 tu kati ya maombi ya wanafunzi 2,500 wenye sifa kutokana na ufinyu wa bajeti.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na kuipongeza Wizara hiyo kwa kazi nzuri iliyofanya katika mwaka uliopita aliitaka Wizara kuzipatia shule zenye maabara wataalamu wa fani hiyo kusaidia na walimu pamoja na wakutubi kwa skuli zenye maktaba.

Wednesday, November 13, 2013

MKUU WA WILAYA HANDENI AWACHARUKIA VIONGOZI WANAOWAOZESHA WASICHANA WA SHULE


MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amewaonya  viongozi watakaojihusisha na kushiriki kuwaozesha wasichana walioko shuleni ya kuwa yeyote atakae bainika amefanya hivyo adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kutokana na wimbi la kuwaozesha wanafunzi wa kike wilayani humo.

Onyo hilo limetolewa  na mkuu wa wilaya  hiyo kwa kusema kuwa hataweza kuvumilia baadhi ya viongozi kushiriki kuwaachisha wasichana shule na kuwatafutia wanaume waolewe kwa kusema kuwa mwanafunzi sio mke aachwe asome kwanza ili wajikomboe kimaisha.

Amesema tayari mtendaji wa Kijiji cha Pozo ameshakamatwa kwa kosa la kushiriki kuwezesha kuolewa kwa mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Pozo ambapo mtendaji huyo alishiriki mchakato mzima wa mwanafunzi huyo hadi kumsafirisha na kumpeleka Dar Es Salaam.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka pia viongozi wa dini kuzingatia sheria za nchi kwa kutowafungisha ndoa  watu ambao wanawasiwasi nao na iwapo watabaini mhusika ni mwanafunzi watoe taarifa haraka katika vyombo husika ili mhusika akamatwa huku akimuagiza afisa elimu wa shule za msingi kufuatilia suala hilo.

Aidha amezitaja shule ambazo zinaongoza kwa utoro wilayani humo kuwa ni shule ya msingi Mazingara,Kweditiribe na Pozo ambapo mkakati wa kuitisha mkutano wa wazazi unafanyika ili kuweza kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu kwa watoto wao.

Monday, October 28, 2013

KAMA ULIMIS PICHA NA MATUKIO YA MAHAFALI YA SHULE YA WASICHA YA ST.CHRISTIINA CHEKI HAPA BAADHI YA SHOW ZILIZOFANYIKA

BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU NA TANO WASICHANA WA SHULE ST.CHRISTINA WAKITOA BURUDANI YA NGOMA KATIKA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULENI HAPO
WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE WA SHULE YA WASICHANA YA ST.CHRISTINA WAKIINGIA UKUMBINI.
UNGEKUWA WW ENGEDONDOSHA NGAPI?

Sunday, October 27, 2013

PICHA NA MATUKIO TOFAUTI YA MAHAFALI YA 9 YA SHULE YA WASICHANA YA ST.CRISTINA

MAANDAMANO YA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE YA SHULE YA WASICHANA YA ST .CRISTINA

MEZA KUU

BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU WAKIIMBA WIMBO WA TANZANIA TANZANIA

MKUU WA SHULE YA WASICHANA YA ST CRISTINA MWALIMU  SINGANO AKIZUNGUMZA MACHACHE KUHUIANA NA SHULE HIYO

BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU WAKITOA BURUDANI YA NGOMA


KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA PANGANI BI HAFSA MTASIWA MEZA KUU AKIPERUZ MACHACHE

DR.NDELAKINDO KESSY MBUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KWENYE MAHAFALI HAYO

BAADHI YA WALIMU WA SHULE YA WASICHANA YA ST.CRISTINA


MGENI RASMI AKIKABIDHI ZAWADI NA VYETI KWA BADHI YA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI

Wednesday, October 23, 2013

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA UZINDUZI WA MAABARA YA SHULE YA LIVING STONE MUHEZA

MKUU WA MKOA WA TANAGA LUTENI MSTAAFU CHIKU GALAWA KUSHOTO,KULIA NI MOJA KATI YA WALIMU WA SHULE HIYO KUTOKA KOREA

MKUU WA MKOA WA TANGA AKIZINDUA JENGO MAAMBARA

MKUU WA MKA WA TANGA AKISOMEWA TAARIFA FUPI YA SHULE HIYO


BAADHI YA WANAFUNZI WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA SHULE HIYO WAKIWA TAYARI KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA TANGA SHULENI HAPO.picha zote kwa hisani ya blog ya Tanga Raha


Monday, October 21, 2013

HALMASHAURI MKOANI TANGA ZAAGIZWA KUJIKITA ZAIDI KWENYE UJENZI WA MAABARA ZA SHULE


NA OSCAR ASSENGA TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ameziagiza Halmashauri zote mkoani hapa kuelekeza msukumo mkubwa kwenye ujenzi wa maabara tatu kila shule ili kuwawezesha wanafunzi kupenda kusoma masomo ya sayansi na kuweza kufanya vizuri.

Gallawa ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea shule ya seminari ya wavulana ya Livingstone iliyopo wilayani hapa pamoja na kuzindua jengo la maabara ya kompyuta  iliyojengwa kwa thamani y ash. 149,000,000 ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ndani.

Amesema ujenzi huo wa maabara kwa vyumba vitatu kila shule ni agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Mrisho Kikwete hivyo kuzitaka halmashauri hizo kutilia mkazo suala hilo kwenye maeneo yao.
Ameongeza kuwa maabara hizo zinapaswa kuwepo kwenye shule za sekondari kuanzia za kata na zile za binafsi kwani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana bila ya kuwepo wanasayansi.

Aidha amesema katika hilo inabidi itumike nguvu kubwa ikiwemo hata kuhairisha miradi mengine ili kuzielekeza kwenye ujenzi wa maabara kwenye shule hizo.

   “Halmashauri zote zinatakiwa kujenga maabara tatu tatu kila shule na sio mbili kwani hilo ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.

Amezitaka halmashauri kupitia ofisa elimu kupita kwenye shule za binafsi kuwasisitizia suala hilo la ujenzi wa maabara kwani ni muhimu sana hasa kwenye maendeleo ya nchi yetu.

Mkuu huyo wa mkoa ameziagiza pia shule za sekondari na msingi mkoani hapa kupanda zao la mkonge kwenye mipaka yao ili kuwezesha wanafunzi kufundishwa jinsi ya kupanda zao hilo.

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA SHULE YA SEKONDARI ELOHIMU

MKU WA WILAYA TANGA HALIMA DENDEGO AKIONESHWA BAADHI YA VIFAA VINAVYOTUMIKA KATIKA MAABARA YA SHULE HIYO KALBA YA MAHAFALI KUANZA


MKURUGENZI WA SHULE YA ELOHIMU BOYS BI ELINGAYA MUNGURE AKITOA HOTUBA YAKE KWA MGENI RASMI

MKUU WA WILAYA YA HALIAMA DENDEGO AKITOA MAELEKEZO KWA WANAFUNZI
BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WA SHULE YA WAVULA NA YA ELOHIMU BOYS WAKIFANYA VITU VYAO

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA KIDATOCHA NNE MLALO SEKONDARI



KATIBU WA UENEZI WA CCM WILAYA YA KOROGWE   BW.RICHARD MGANGA ALIYEMUAKILISHA MWENYEKITI WA CCM MKOA KATIKA MAHAFALI HAYO KUSHOTONI MKUU WA SHULE HIYO SUFIANI SHEKOLOLA




BAADHI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAKIONESHA VITU VYAOMBELE YA MGENI RASMI




MMOJA WA WALIMU WANAOFUNDISHA SHULENI HAPO BW SULTANI



 
KATIBU WA UENEZI CCM WILAYA YA KOROGWE BW..MGANGA KUSHOTO,KULIA NI MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM WILAYANI LUSHOTO WAKIENDESHA HARAMBEE SHULENI HAPO



BAADHI YA WATU WALOHUDHURIA MAHAFALI HAYO








ELIMU BADO CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI ELOHIMU BOYS



Licha ya shule ya sekondari ya wavulana ya Elohim kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma inakabiliwa na changamoto ya wanafunzi wengi kushindwa kujitambua na  kuona suala zima la kusoma kama mzingo waliotishwa na wazazi wao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Jofrey Makanza wakati akisoma hotuba yake kwa mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego kwenye mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya shule hiyo.

Makanza amesema suala lengine ambalo limekuwa kikwazo kwao ni wazazi,walezi kushindwa kulipa ada zao kwa wakati na kueleza jinsi wanavyokabiliana nayo likiwemo la kuwakumbusha wazazi kutimiza wajibu wao ikiwemo kuwarudisha nyumbani.

Amesema wanafunzi wanaoshindwa kuonesha uendelevu wa kitaaluma kwa kiwango kinachostahili hupewa ushauri unaostahili na walimu wakishirikiana na wazazi wao ili kupata wahitimu bora na sio bora wahitimu sanjari na mkakati wa serikali wa Big result now.

Aidha ameishukuru serikali kwa mikakati mbalimbali ya kielimu inayoiweka ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa watoto hususani kurejeshwa mitihani ya kidato cha pili.