Search This Blog

Monday, December 30, 2013

IDARA YA UKAGUZI IBORESHWE KUNUSURU ELIMU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu (CCM          
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Betty Machangu (CCM), ameishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuangalia na kuboresha Idara ya Ukaguzi ili kuipa makali ili itembelee na kukagua shule zilizopo mikoani na siyo kuishia mijini.

Akizungumza na wandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Machangu alisema kama serikali inataka kukuza kiwango cha elimu, ni lazima iangalie namna ya kuboresha ukaguzi kwani ndiyo roho ya elimu nchini.
“Watu wanaongea kuhusu mitaala ya elimu na mambo mengine ila nataka kuwaambia kama Idara ya Ukaguzi kama haitapewa fedha za kutosha ili iweze kwenda vijijini ni sawa na bure,” alisema Machangu.

Machangu alisema: “Ukifutilia shule nyingi hapa nchini utakuta zina vyoo visivyokuwa na uwezo kutumiwa na binadamu pamoja na walimu kutoudhuria madarasani, yote hayo yanachangia elimu kushuka na tusitegemee miujiza katika elimu.”

Machangu alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku nne tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu.
SOURCC Nipashe

No comments:

Post a Comment