Search This Blog

Sunday, December 1, 2013

SHULE 10 SEKONDARI ARUSHA ZAULA TEKNOHAMA















Shule 10 za sekondari za serikali mkoani hapa zinatarajiwa kuunganishwa bure na huduma za intaneti yenye kasi ya 4G LTE  ili  kuinua uelewa wa wanafunzi katika somo la Teknolojia ya Habari (Teknohama).

Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mtandao wa huduma za Fouth Generation Long Term Evolution jijini hapa, mkurugenzi  wa kampuni Smile Communication kwa Tanzania na Uganda, Fiona Mcgloin, alisema kwa

kuanzia wamewaunganishia huduma hiyo Shule ya Sekondari ya Arusha baada ya uzinduzi uliofanyika juzi.

Alisema kama sehemu ya mpango wa kuwajibika kijamii wa kampuni hiyo, inatoa huduma za bure za intaneti yenye kasi katika shule za serikali na kwamba hadi sasa shule 10 za jijini Dar es Salaam zinanufaika na huduma hiyo na kuna mpango kama huo kufanyika mkoani hapa.

Aidha alisema wanatarajia kufanya hivyo kwa mikoa yote ambayo watakayozindua huduma hiyo.

Alisema wapo tayari kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya biashara zilizopo mkoani hapa na kuwapa kazi wakazi wa jiji.

Alisema mtandao huo utawasaidia wafanyabiashara, watalii na sekta ya elimu ambayo kwa kiasi kikubwa Arusha imekuwa kitovu.

Alisema Smile ilizinduliwa Dar es Salaam Mei 16, mwaka huu na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mapinduzi haya ya teknolojia.

Katika sekta inayokua kwa kasi ya mawasiliano hapa nchini, intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara nne zaidi kuliko 3.75G.
Source Nipashe

No comments:

Post a Comment