Search This Blog

Wednesday, November 13, 2013

MKUU WA WILAYA HANDENI AWACHARUKIA VIONGOZI WANAOWAOZESHA WASICHANA WA SHULE


MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amewaonya  viongozi watakaojihusisha na kushiriki kuwaozesha wasichana walioko shuleni ya kuwa yeyote atakae bainika amefanya hivyo adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kutokana na wimbi la kuwaozesha wanafunzi wa kike wilayani humo.

Onyo hilo limetolewa  na mkuu wa wilaya  hiyo kwa kusema kuwa hataweza kuvumilia baadhi ya viongozi kushiriki kuwaachisha wasichana shule na kuwatafutia wanaume waolewe kwa kusema kuwa mwanafunzi sio mke aachwe asome kwanza ili wajikomboe kimaisha.

Amesema tayari mtendaji wa Kijiji cha Pozo ameshakamatwa kwa kosa la kushiriki kuwezesha kuolewa kwa mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Pozo ambapo mtendaji huyo alishiriki mchakato mzima wa mwanafunzi huyo hadi kumsafirisha na kumpeleka Dar Es Salaam.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka pia viongozi wa dini kuzingatia sheria za nchi kwa kutowafungisha ndoa  watu ambao wanawasiwasi nao na iwapo watabaini mhusika ni mwanafunzi watoe taarifa haraka katika vyombo husika ili mhusika akamatwa huku akimuagiza afisa elimu wa shule za msingi kufuatilia suala hilo.

Aidha amezitaja shule ambazo zinaongoza kwa utoro wilayani humo kuwa ni shule ya msingi Mazingara,Kweditiribe na Pozo ambapo mkakati wa kuitisha mkutano wa wazazi unafanyika ili kuweza kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu kwa watoto wao.

No comments:

Post a Comment