SHULE za msingi za Qash na Dudiye zilizopo wilayani Babati mkoani Manyara zimetajwa kutokuwa na vyoo tangu mwaka 2006 hadi sasa na badala yake wanafunzi mapori yaliyo jirani na shule kwa ajili ya kujisaidia.
Hayo yamebainika wakati wa kikao cha mrejesho wa kampeni ya ya uwajibikaji jamii ilichoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Eraston Mbwilo ni baada ya maofisa wa Shirika la Haki elimu kutembelea baadhi ya shule za msingi wilayani humo na kujionea hali halisi katika shule hizo.
Akitoa marejesho katika kampeni hiyo, Asia Lembariti amesema kwamba shule hizo hazina matundu ya vyoo tangu mwaka 2006 hadi sasa hali ambayo inatia wasiwasi kwa kuibuka kwa magonjwa ya kuhara na kichocho.
Nae Ofisa Elimu wa Shule za msingi, Mery Consolata amekiri kutokuwepo kwa miundo mbinu katika shule hizo hasa vyoo,vyumba vya madarasa na walimu na kusema kwamba wazazi na walimu wanapaswa kushirikiana ili kuweza kuondokana hali hiyo ya muda mrefu.

No comments:
Post a Comment