Wanafunzi
waliomaliza mitihani yao ya darasa la saba wameiomba serikali kuboresha kambi
walizokuwa wamewawekea kufundishwa ziendelezwe hadi shule za sekondari.
Wakizungumza na Mimi na Mwanafunzi baada ya kumaliza mtihani wa mwisho wanafunzi wa shule ya msingi Chanika wilayani Handeni mkoani Tanga wameshukuru kambi hizo kwani zimekuwa na faida kwao katika mitihani waliofanya.
Rashidi Rajabu mwanafunzi wa shule ya msingi Chanika amesema kuwa kambini walikuwa wakifanya majaribio mara kwa mara hali iliyowafanya kujiongezea ujasiri wakutoogopa mitihani.
Akiongelea suala hilo Afisa Taaluma Sekondari wilaya ya Handeni, Basil Mrutu amesema mpango huo wa kuanzisha kambi hizo kwa sekondari katika robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha 2013-2014 kwa sekondari zote za sekondari wilayani humo upon a utaanza.
Mrutu amewaomba wazazi
washirikiane na viongozi wa shule katika kutoa chakula cha mchana kwa kuchangia
fedha kidogo ili wanafunzi wapate chakula shuleni.
No comments:
Post a Comment