Search This Blog

Friday, September 6, 2013

BAVARIA YADHAMINI MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGERZA KWA WANAFUNZI MKOA WA TANGA

















OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


BAADHI YA WANAFUNZI WALIOKUWA WAMEHUDHURIA
 KWENYE MASHINDANO HAYO


 
OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI  AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO KULIA NA KUSHOTO KWAKE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,MUSTAPHA SELLEBOSS WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO.

Campuni ya kinywaji baridi  cha Bavaria Jovet T imeamua kufadhili mashindano ya lugha ya kingereza mkoa wa Tanga  ili kuleta hamasa zaidi katika elimu na kuunga mkono harakati zote zinazofanywa na wadau wa sekta ya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari Operation Manaje wa Jovet (T)Limited Catherine Munguti ambae alimuwakialisha Managing Director John kessy kwenye hafla hiyo amesema kuwa mashindano hayo  yatakuwa endelevu kwa mikoa yote na wameanza na Tanga kama kitovu.

Amesema kutokana na kutambua umuhimu wa elimu elimu mashindano hayo ya lugha ya kiingereza watayapeleka kila mkoa ili kuhamasisha zaidi wanafunzi kujifunza na kuzungumza lugha ya kiingereza  hivyo kuziomba shule za sekondari za mikoa mingine kujiandaa.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa kamati ya  Uchumi, Afya elimu Halmashauri ya jiji la Tanga Mustapha Seleboss ambae pia ni Diwani wa kata ya Nguvumali amesema mashindano hayo ni mazuri licha kuwa kumejitokeza baadhi ya changamoto zikiwemo za   baadhi ya shule kutokufika katika mashindano hayo huku baadhi ya wanafunzi wakionekana kupata ugumu juu ya lugha ya kingereza.

Seleboss ametoa kauli hiyo mapema wiki hii  wakati akifungua mashindano ya kwanza ya ‘Bavaria Malt English’ kwa ajili ya shule za sekondari za Tanga yaliyojumuisha wanafunzi kutoka shule 22 za mkoani humo huku akiahidi Halmashauri ya jiji la Tanga itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau katika masuala ya elimu.



No comments:

Post a Comment