Search This Blog

Wednesday, February 26, 2014

HUU NDO MNARA WA SHULE MAMA JIJINI TANGA


Huu ni mnara uwa shule ya sekondari ya Tanga school iliyoanzishwa mwaka 1895 chini ya utawala wa kijerumani ambapo shule hiyo mwanzo ilijengwa eneo la mkwakwani ambapo sasa ipo shule ya sekondari ya old Tanga

Wednesday, January 22, 2014

SHULE YAAMUA KUFANYA MONITORNG KUSIMAMIA MITIHANI

Shule moja ya nchini Ubelgiji imeamua kutumia ndege isiyo na rubani (drone) kusimamia mitihani baada ya kushindwa mbinu za kawaida kuwazuia wanafunzi kufanya udanganyifu katika mitihani yao.

Ndege hiyo ina kamera ya kuchukua picha za video pamoja na kurekodi harakati yoyote inayotia wasiwasi kutoka kwa mwanafunzi yeyote yule na kurusha moja kwa moja kwenye TV moja kubwa, harakati yoyote ile isiyo ya kawaida ya wanafunzi.
  ZIDI CHEKI VIDEO HAPO CHINI
Source radio tehrani

Wednesday, January 1, 2014

WILAYA YA TANGA UFAULU MATOKEO YA LASABA WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 40


Wilaya ya Tanga katika mwaka huu wa 2013 mefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kwa ufaulu wa wanafunzi wa  darasa la saba ambao walifanya mtihani wao wa Taifa mwezi wa kumi  ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

Akizungumza ofisini kwake kaimu Afisa elimu Jiji, Damas Kifanga alisema kuwa ufaulu huo uliojumuisha shule 93 za Tanga mjini na Vijijini  umeongezeka mwaka huu ingawa sekta hiyo ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi.

Aidha alisema katika sekta hiyo ya elimu Wilaya ya Tanga mwaka huu imefanikiwa kutoa wanafunzi 4266 kati ya wanafunzi 6261 sawa na 40% ya ufaulu wa matokeo ya darasa la saba ambapo ni tofauti na mwaka jana kitu ambacho kinaleta hamasa katika sekta hiyo muhimu katika maisha ya kila siku.

Hata hivyo Kifanga alisema kuwa ili kukabiliana na idadi ndogo ya wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na shule za serikali,ni lazima kuunganisha nguvu kutoka serikalini,wazazi na taasisi zisizo za kiserikali ili kuweza kuinua sekta hiyo ya elimu katika Wilaya ya Tanga Mjini.

Alisema kuwa upo umuhimu wa utolewaji wa chakula mashuleni ili kuboresha mahudhurio na kuwepo na usikivu mzuri wa wanafunzi pindi wawapo madarasani kitu ambacho bado kinasuasua kwa baadhi ya shule na kupelekea kufikia malengo mazuri waliojiwekea.

Kifanga alizidi kusema kuwa uboreshwaji wa mindombinu ni muhimu katika sekta hiyo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika baadhi ya shule kitu ambacho kwa namna moja au nyingine kinaweza kupunguza umakini kwa wanafunzi wawapo katika masomo yao.

Bwana Kifanga alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuongeza jitihada katika utowaji wa fedha za uwendeshaji wa shughuli zote za elimu na kuwa saidia kukamilisha  kwa wakati miundombinu amabyo wananchi wanayanzisha kwa nguvu zao katika kuboresha elimu Wilayani humu.

Ameiomba serikali kuwa  Halmashauri  zinapaswa kuboreshewa uewzo wa kifedha  ili kuweza kusaidia mafunzo ya walimu waliopo makazini ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi wa kielimu.

Monday, December 30, 2013

IDARA YA UKAGUZI IBORESHWE KUNUSURU ELIMU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu (CCM          
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Betty Machangu (CCM), ameishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuangalia na kuboresha Idara ya Ukaguzi ili kuipa makali ili itembelee na kukagua shule zilizopo mikoani na siyo kuishia mijini.

Akizungumza na wandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Machangu alisema kama serikali inataka kukuza kiwango cha elimu, ni lazima iangalie namna ya kuboresha ukaguzi kwani ndiyo roho ya elimu nchini.
“Watu wanaongea kuhusu mitaala ya elimu na mambo mengine ila nataka kuwaambia kama Idara ya Ukaguzi kama haitapewa fedha za kutosha ili iweze kwenda vijijini ni sawa na bure,” alisema Machangu.

Machangu alisema: “Ukifutilia shule nyingi hapa nchini utakuta zina vyoo visivyokuwa na uwezo kutumiwa na binadamu pamoja na walimu kutoudhuria madarasani, yote hayo yanachangia elimu kushuka na tusitegemee miujiza katika elimu.”

Machangu alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku nne tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu.
SOURCC Nipashe

Sunday, December 15, 2013

PICHA ZA MAHAFALI YA 19 DSJ HIZI HAPA

Meza kuu
Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka hu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawaziliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.

Baadhi ya wahitimu wakibadilishana mawili matatu


Dotto, Abushehe Nondo, Ibrahim Yamola na Juliana Malondo



Sunday, December 1, 2013

SHULE 10 SEKONDARI ARUSHA ZAULA TEKNOHAMA















Shule 10 za sekondari za serikali mkoani hapa zinatarajiwa kuunganishwa bure na huduma za intaneti yenye kasi ya 4G LTE  ili  kuinua uelewa wa wanafunzi katika somo la Teknolojia ya Habari (Teknohama).

Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mtandao wa huduma za Fouth Generation Long Term Evolution jijini hapa, mkurugenzi  wa kampuni Smile Communication kwa Tanzania na Uganda, Fiona Mcgloin, alisema kwa

kuanzia wamewaunganishia huduma hiyo Shule ya Sekondari ya Arusha baada ya uzinduzi uliofanyika juzi.

Alisema kama sehemu ya mpango wa kuwajibika kijamii wa kampuni hiyo, inatoa huduma za bure za intaneti yenye kasi katika shule za serikali na kwamba hadi sasa shule 10 za jijini Dar es Salaam zinanufaika na huduma hiyo na kuna mpango kama huo kufanyika mkoani hapa.

Aidha alisema wanatarajia kufanya hivyo kwa mikoa yote ambayo watakayozindua huduma hiyo.

Alisema wapo tayari kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya biashara zilizopo mkoani hapa na kuwapa kazi wakazi wa jiji.

Alisema mtandao huo utawasaidia wafanyabiashara, watalii na sekta ya elimu ambayo kwa kiasi kikubwa Arusha imekuwa kitovu.

Alisema Smile ilizinduliwa Dar es Salaam Mei 16, mwaka huu na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mapinduzi haya ya teknolojia.

Katika sekta inayokua kwa kasi ya mawasiliano hapa nchini, intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara nne zaidi kuliko 3.75G.
Source Nipashe

Tuesday, November 26, 2013

NIKI WA PILI ASEMA NENO KUHUSU WANAFUNZI!

Raper artist kutoka kundi la weusi Niki wa pili amewataka wanafunzi Tanzania kusoma kwa bidii na kutokata tamaa ya kimaisha.

Kauli hiyo ya niki wa pili inakuja baada ya kuulizwa swali juu ya nini anafikiri mara baada ya kumaliza degree yake ya pili ya Managment devolopment wiki iliyopita.

Niki amewataka wanafunzi kutambua umuhimu wa elimu licha ya kuwa wengi hukata tamaa kutokana na mikakati yao kuwa katika hali duni.

Hata hivyo niki amesema kusoma si kugumu na kinachotakiwa ni kupenda na kuweka juhudi kwa kuzingatia uchaguzi sahihi wa masomo wa mwanafunzi atakayoweza kuyamudu.

 "Uki sooma elimu itakupa uwanja mpana katika maisha yako na itakuongezea heshima na thamani ya maisha yako"Alisema niki wa pili

Niki ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum kupitia kituo cha redio mwambao fm Tanga mapema hii leo kupitia kipindi cha mimi na mwanafunzi kinarushwa redioni hapa.