Search This Blog

Tuesday, November 26, 2013

NIKI WA PILI ASEMA NENO KUHUSU WANAFUNZI!

Raper artist kutoka kundi la weusi Niki wa pili amewataka wanafunzi Tanzania kusoma kwa bidii na kutokata tamaa ya kimaisha.

Kauli hiyo ya niki wa pili inakuja baada ya kuulizwa swali juu ya nini anafikiri mara baada ya kumaliza degree yake ya pili ya Managment devolopment wiki iliyopita.

Niki amewataka wanafunzi kutambua umuhimu wa elimu licha ya kuwa wengi hukata tamaa kutokana na mikakati yao kuwa katika hali duni.

Hata hivyo niki amesema kusoma si kugumu na kinachotakiwa ni kupenda na kuweka juhudi kwa kuzingatia uchaguzi sahihi wa masomo wa mwanafunzi atakayoweza kuyamudu.

 "Uki sooma elimu itakupa uwanja mpana katika maisha yako na itakuongezea heshima na thamani ya maisha yako"Alisema niki wa pili

Niki ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum kupitia kituo cha redio mwambao fm Tanga mapema hii leo kupitia kipindi cha mimi na mwanafunzi kinarushwa redioni hapa.

Saturday, November 23, 2013

MWASITY AWATOA HOFU WANAFUNZI TANGA



































Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mdau wa mausuala ya elimu hapa nchini Mwasiti Almas a.k.a mwasiti amewatoa hofu wanafunzi wa mkoa wa Tanga juu ya kuchelewa kwa tour za kampeni ya tokomeza zero.

Mwasity ametoa kauli hiyo  kutoka na kuonekana kuchelewa kwa tour za kampeni hizo zilijulikanazo kama tokomeza zero.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu kwenye kipindi cha Mimi na Mwanafunzi kinachorushwa na Redio Mwambao fm ya Tanga Msanii huyo amesema kampeni hiyo ya uhamasishaji na uelimishaji juu ya wanafunzi kusoma kwa biidii na kuepuka matokeo mabaya inaendelea.

Hata hivyo mwasiti amesema safari za kuzunguka kwa ajili ya uhamasishaji na ulimishaji juu ya kampeni hiyo mashuleni zimechelewa kuanza mapema kutokana na wasanii walioshiriki katika kampeni hiyo wengi kumalizia project zao mbalimbali za kimziki mwishoni mwa mwaka na kampeni hiyo itaanza rasmi mwezi januari.

Aidha amewataka wanafunzi mkoani Tanga kusoma kwa bidii na kuwa tayari kwa ajili ya kampeni hiyo itakayo ambatana na utambuzi wa makundi mbalimbali ya wanafunzi watakayo yatengeneza kwa ajili ya uhamasishaji na uelimishaji juu ya kampeni hiyo..

Wednesday, November 20, 2013

WALIMU WAJA NA MBINU MPYA


 Baadhi ya walimu mkoani Tanga wamebuni namna mpya ya kuwafundisha wanafunzi wao kirahisi baada ya vitabu vya somo husika kuwa vichache chek hii hapa walimu wameamua kuandika table ya somo la chemisrty ukutani ili kuwapa wanafunzi unafuu zaidi wa kukariri
HAYA WALE WAKALI WA CHEMISTRY

Monday, November 18, 2013

SHULE ZAKOSA VYOO BABATI


SHULE  za msingi za Qash na Dudiye zilizopo wilayani Babati mkoani Manyara zimetajwa kutokuwa na vyoo tangu mwaka 2006 hadi sasa na badala yake wanafunzi mapori yaliyo jirani na shule kwa ajili ya kujisaidia.

Hayo yamebainika wakati wa kikao cha mrejesho wa kampeni ya ya uwajibikaji jamii ilichoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Eraston Mbwilo ni baada ya maofisa wa Shirika la Haki elimu kutembelea baadhi ya shule za msingi wilayani humo na kujionea hali halisi katika shule hizo.

Akitoa marejesho katika kampeni hiyo, Asia Lembariti amesema kwamba shule hizo hazina matundu ya vyoo tangu mwaka 2006 hadi sasa hali ambayo inatia wasiwasi kwa kuibuka kwa magonjwa ya kuhara na kichocho.

Nae Ofisa Elimu wa Shule za msingi, Mery Consolata amekiri kutokuwepo kwa miundo mbinu katika shule hizo hasa vyoo,vyumba vya madarasa na walimu na kusema kwamba wazazi na walimu wanapaswa kushirikiana ili kuweza kuondokana hali hiyo ya muda mrefu.

BODI YA MIKOPO YATAKIWA KUONGEZA KASI ZANZIBAR


Na masanja Mabula Zanzibar
Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu Zanzibar imetakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni kutoka kwa wahitimu waliokopeshwa na Bodi hiyo ili kuongeza uwezo wa Bodi kutoa mikopo zaidi kwa wanafunzi.

Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati akihitimisha Kikao cha Kutathmini Utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwaka 2012/2013 na robo ya kwanza ya mwaka 2013/2014.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo katika bajeti ya mwaka wa fedha uliopita zilihitajika jumla ya shilingi bilioni 7.7 kulipia wanafunzi 1012 wa zamani na wanafunzi wapya 881 pamoja na madeni ya nyuma.

Kwa upande wa mwaka wa fedha 2013/2014 taarifa imeonyesha kuwa Bodi hiyo imeweza kuwadhamini wanafunzi 1,300 tu kati ya maombi ya wanafunzi 2,500 wenye sifa kutokana na ufinyu wa bajeti.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na kuipongeza Wizara hiyo kwa kazi nzuri iliyofanya katika mwaka uliopita aliitaka Wizara kuzipatia shule zenye maabara wataalamu wa fani hiyo kusaidia na walimu pamoja na wakutubi kwa skuli zenye maktaba.

Wednesday, November 13, 2013

MKUU WA WILAYA HANDENI AWACHARUKIA VIONGOZI WANAOWAOZESHA WASICHANA WA SHULE


MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amewaonya  viongozi watakaojihusisha na kushiriki kuwaozesha wasichana walioko shuleni ya kuwa yeyote atakae bainika amefanya hivyo adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kutokana na wimbi la kuwaozesha wanafunzi wa kike wilayani humo.

Onyo hilo limetolewa  na mkuu wa wilaya  hiyo kwa kusema kuwa hataweza kuvumilia baadhi ya viongozi kushiriki kuwaachisha wasichana shule na kuwatafutia wanaume waolewe kwa kusema kuwa mwanafunzi sio mke aachwe asome kwanza ili wajikomboe kimaisha.

Amesema tayari mtendaji wa Kijiji cha Pozo ameshakamatwa kwa kosa la kushiriki kuwezesha kuolewa kwa mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Pozo ambapo mtendaji huyo alishiriki mchakato mzima wa mwanafunzi huyo hadi kumsafirisha na kumpeleka Dar Es Salaam.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka pia viongozi wa dini kuzingatia sheria za nchi kwa kutowafungisha ndoa  watu ambao wanawasiwasi nao na iwapo watabaini mhusika ni mwanafunzi watoe taarifa haraka katika vyombo husika ili mhusika akamatwa huku akimuagiza afisa elimu wa shule za msingi kufuatilia suala hilo.

Aidha amezitaja shule ambazo zinaongoza kwa utoro wilayani humo kuwa ni shule ya msingi Mazingara,Kweditiribe na Pozo ambapo mkakati wa kuitisha mkutano wa wazazi unafanyika ili kuweza kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu kwa watoto wao.