Search This Blog

Thursday, February 28, 2013

LAWAMA HAZISAIDII DHIDI YA MATOKEO SHIRIKIANENI NA WALIMU MJUE MTAFANYA NINI




WAZAZI  wametakiwa kuacha tabia ya kulalamika hasa wanapoona matokeo
ya mithiani ya kitaifa yamekuwa mabaya na badala yake wanatakiwa
kutafuta mbinu ambazo watashirikiana na walimu ili kuweza kuokoa wimbi
kubwa la watoto ambao wanashindwa kufanya vema katika mithiani ya
mwisho
Asilimia kubwa ya wazazi wao wanapenda kutoa lawama kwa walimu  na
hata wakati mwingine kwa Serikali bila kujua kuwa wao wana nafasi
kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto wao pindi wanapokuwa mashulenina hata kabla hawajafanya mithiani yao ya mwisho

Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Mkuu wa shule ya Sekondari ya
Arusha Modern,Philiph Wasike wakati akiongea na wanafunzi pamoja na
wazazi katika maafali ya Saba ya kidato cha sita shuleni hapo.

Wasike alisema kuwa lawama ambazo wanatoa wazazi hasa wanapoona
matokeo ya mwisho   ni mabaya kamwe hayataweza kuwasadia na badala
yake ndio yanazidi kuangamiza watoto,hivyo basi wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanabuni mbinu ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi wao
Aliongeza kwa kutolea mfano kuwa kwa sasa asilimia kubwa sana ya
wazazi wanawaza jinsi ya kulipa ada lakini hawawazi jinsi ya
kuwasaidia wanafunzi  hasa wale wenye uelewa mdogo hivyo mzigo huo
unaachiwa kwa walimu  pamoja na uongozi wa shule ambao wakati mwingine nao unalemewa kwa kuwa hakuna msaada kuutoka kwa wazazi
“matokeo ya kidato cha nne yaliyoytangazwa wiki iliyopita watoto
wamefeli sana lakini kila mzazi analaumu bila ya kujua kuwa nao wao ni
chanzo kikubwa sana kwa kuwa wazazi wengi sana wanawaza jinsi ya
kupata ada hawawazi jinsi ya kuwasaidia na kuwapa moyo wanafunzi sasa
ni vema kila mzazi kabla hajatanguliza lawama mbele kwanza wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanafuatilia maendeleo ya wanafunzi wao kwa ukaribu
sana”aliongeza Wasike

Katika Hatua nyingine alisema kuwa nayo Serikali inatakiwa kuhakikisha
kuwa inajiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanaboresha zadii sekta
ya elimu kwa kuhakikisha kuwa walimun wanakuwa na maslahi mazuri ili
walimu nao waweze kuwa na moyo pindi wanapowafundisha wanafunzi
Pia alisema kuwa hata walimu wanapokosa maslahi mazuri kuna changia
kwa kiwango cha hali ya juu sana washinde kufundisha kwa Moyo hali
ambayo kwa wakati mwingine inasababisha wanafunzi wafanye vibaya
katika mithiani yao ya mwisho hali ambayo wakati mwingine inaongeza
Mbumbumbu kwenye taifa
‘sekta ya elimu ni moja ya sekta ambazo zinatakiwa kupewa kipaumbele
kikubwa sana ikiwa ni pamoja na kuangalia hata mazingira ya
kufundishia kwa kuwa hata wakati mwingine mazingira nayo yanakuwa ni
magumu sana sasa tunapolalamika kuwa matokeo ni mabaya ni lazima
tuangalie vyanzo ni nini na wala sio kumtafuta mchawi wa matokeo ni
nani”alibainisha Wasike



Hatuna mpango wa kuwasaidia waliofeli kidato cha lV-Mulugo















Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema wizara haina mpango wowote kwa sasa kuhusiana na wanafunzi waliofeli kidato cha nne mpaka pale Tume itakapomaliza kufanya kazi yake ndipo itaamua nini cha kufanya.

Mulugo alikiambia chanzo hiki kuwa wizara inasubiri Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imalize kufanya kazi yake, ndipo itatoa uamuzi nini kifanyike juu ya wanafunzi hao.

“Kwa sasa siwezi nikasema chochote kwani tume imeundwa ili kulifanyia kazi jambo hilo, hivyo tunasubiri wamalize kufanya kazi yao ndipo tutatoa kauli ya nini kifanye juu ya wanafunzi walio feli kama ni kurudia tena mtihani au la,” alisema Mulugo.

Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa wizara yake inazungumziaje juu ya mpango wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kuandaa mafunzo ya kozi ya muda mfupi kwa vijana wote waliofeli mkoani humo ili kuwapima kama wapo wanaaoweza kusaidiwa kuendelea na elimu ya cheti.

Msambatavangu alitoa uamuzi huo baada ya makubaliano yake na baadhi ya vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Tumaini (IUCO) na Chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) na kukubaliana kutoa mafunzo hayo yatakayo anza Machi mwaka huu. 

Mulogo alisema kuwa ni wazo lenye mpango mzuri wa kuwasaidia vijana wengi ambao ni kama wamekumbwa na tatizo kwa sasa, hivyo anacho kifanya Mwenyekiti huyo hakina madhara yoyote  na anafanya kama raia mwema aliyeguswa na matokeo hayo